NAFASI 50 Za Internship Sokoine University of Agriculture 2025/2026

NAFASI 50 Za Internship Sokoine University of Agriculture 2025/2026
NAFASI 50 Za Internship Sokoine University of Agriculture 2025/2026
AJIRA 50 Za Muda (Internship) Kupitia Programu Maalum ya Kuendeleza Zao la Korosho nchini.
Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo (MoA) na Bodi ya Korosho (CBT) Kinatekeleza programu ya kushirikisha vijana katika kilimo ya Jenga Kesho iliyo bora katika zao la Korosho (Building a Better tomorrow- BBT-Korosho).
Katika mpango wa BBT-Korosho, SUA-MoA-CBT imeandaa mpango wa kuajiri kwa muda kupitia shughuli za kukuza ujuzi (internship) wa mwaka mmoja maafisa Ugani Kilimo na maafisa Ugani Wasaidizi 50 kwa ajili ya programu maalum ya kuendeleza zao la korosho nchini.
Mpango utatekelezwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2025/2026 ikiwa ni maandalizi ya uzalishaji wa korosho ghafi.
Mpango huu utatekelezwa katika mikoa ya Mtwara, Lindi,Ruvuma (Tunduru) na Pwani.
Kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha huduma za ugani hapa nchini, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na SUA na wadau wengine wa kilimo katika kutekeleza program hii maalum ya huduma za ugani kupitia vijana wahitimu katika fani za kilimo (BBT Agricultural Extension Entrepreneurship Scheme- BBT AEES).
Kupitia BBT-AEES nafasi hamsini (50) zinahitajika kujazwa na wahitimu wenye sifa stahiki katika fani za kilimo ili kutoa huduma za ugani katika zao la Korosho kwa utaratibu wa ajira za muda (internship) kama ifuatavyo:-
✅AFISA KILIMO/ (NAFASI 10)
MAJUKUMU YA MUHIMU NI PAMOJA NA:
(a)Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa zao la korosho kwa kufanya yafuatayo:-
- Kutoa elimu ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima kuanzia kuandaa shamba, kutunza shamba, kuvuna, kuongeza thamani, kuhifadhi hadi kuuza sokoni.
- Kutoa elimu na kusimamia ubora wa korosho ghafi kuanzia shambani hadi ghalani.
- Kufuatilia na kuhakikisha kuwa wakulima wanazingatia Kanuni za kilimo bora cha korosho.
- Kuandaa na kutoa taarifa kila wiki kuhusu maendeleo ya kilimo cha korosho katika eneo husika la kazi.
- Kuandaa mahitaji halisi ya pembejeo ikiwa ni pamoja na mbegu/miche kwa wakulima na kuwasilisha Bodi ya Korosho Tanzania.
- Kusimamia na kuhakikisha pembejeo zilizosambazwa katika eneo husika zinawafikia wakulima na wanazitumia katika mashamba yao ya mikorosho.
(b) Kuhuisha kanzidata ya wakulima wa korosho na wadau wengine ikiwemo watoa huduma za pembejeo katika eneo lake kwenye mfumo wa kidijitali uliopo.
(c)Kusimamia ugawaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho zinazotolewa na Serikali kwa wakulima wa korosho katika eneo lake la kazi.
(d)Kutoa mafunzo ya kilimo bora cha korosho ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu kwa wakulima.
(e)Kusimamia uhakiki wa ubora wa korosho katika ngazi ya Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS).
(f)Kuanzisha mashamba ya mfano na shamba darasa katika eneo la kazi.
(g)Kuandaa makadirio ya uzalishaji wa korosho ghafi kwa kuzingatia kigezo cha miti ya mikorosho iliyopo yenye uwezo wa kuzalisha katika msimu husika (Crop forecast).
(h)Kukusanya taarifa/takwimu za korosho zinazobanguliwa majumbani/vikundi vidogo
vya ubanguaji na kuwasilisha Bodi ya Korosho Tanzania.
(i)Kuwatambua wadau wa sekta ya kilimo waliopo katika eneo husika la kazi na kuwaunganisha na wakulima ili kupata huduma wanazotoa.
(j)Kuhakikisha kila mkulima ana daftari ambalo litatumika kujaza huduma zitakazotolewa na wadau mbalimbali wakiwemo maafisa ugani kilimo.
(k)Kushirikiana na uongozi wa kijiji kuchagua mkulima kiongozi (Lead farmer).
(l)Kutoa ushauri kwa mazao mengine yanayolimwa na wakulima wa Kijiji/eneo analosimamia.
(m)Kufanya tathmini ya uzalishaji na ubanguaji wa korosho katika eneo lake la kazi kila mwisho wa msimu na kuwasilisha taarifa kwa Bodi ya Korosho Tanzania.
(n)Kusimamia maafisa ugani wasaidizi katika eneo husika.
(o)Kufanya shughuli nyingine yoyote atakayopangiwa na kiongozi wake.
Sifa zinazohitajika Kijana muhitimu wa fani ya kilimo ngazi ya shahada (Degree) mwenye sifa zifuatazo:-
- Awe mtanzania mwaminifu, mwadilifu, mwenye kujituma na mahusiano mazuri na
wengine. - Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40.
- Awe amehitimu shahada (Degree) katika fani ya Sayansi ya Kilimo (Agriculture General), Agronomia (Agronomy), Kilimo cha Bustani (Horticulture) au Uzalishaji wa
Mazao (Crop Production) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali. - Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma.
- Awe hajawahi kufungwa kwa makosa yoyote ya jinai.
- Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa..Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba.
- Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika.
- Uzoefu wa kazi katika zao la korosho ni sifa ya ziada.
✅AFISA KILIMO MSAIDIZI (NAFASI 40)
MAJUKUMU YA MUHIMU NI PAMOJA NA:
a)Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa zao la korosho kwa kufanya yafuatayo:-
- Kutoa elimu ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima kuanzia kuandaa shamba, kutunza shamba, kuvuna, kuongeza thamani, kuhifadhi hadi kuuza sokoni.
- Kutoa elimu na kusimamia ubora wa korosho ghafi kuanzia shambani hadi ghalani.
- Kufuatilia na kuhakikisha kuwa wakulima wanazingatia Kanuni za kilimo bora cha korosho.
- Kuandaa na kutoa taarifa kila wiki kuhusu maendeleo ya kilimo cha korosho katika eneo husika la kazi.
- Kuandaa mahitaji halisi ya pembejeo ikiwa ni pamoja na mbegu/miche kwa wakulima na kuwasilisha Bodi ya Korosho Tanzania.
- Kusimamia na kuhakikisha pembejeo zilizosambazwa katika eneo husika zinawafikia wakulima na wanazitumia katika mashamba yao ya mikorosho.
b)Kuhuisha kanzidata ya wakulima wa korosho na wadau wengine ikiwemo watoa huduma za pembejeo katika eneo lake kwenye mfumo wa kidijitali uliopo.
c)Kusimamia ugawaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho zinazotolewa na Serikali kwa wakulima wa korosho katika eneo lake la kazi.
d)Kutoa mafunzo ya kilimo bora cha korosho ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu kwa wakulima.
e)Kusimamia uhakiki wa ubora wa korosho katika ngazi ya Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS).
f)Kuanzisha mashamba ya mfano na shamba darasa katika eneo la kazi.
g)Kuandaa makadirio ya uzalishaji wa korosho ghafi kwa kuzingatia kigezo cha miti ya mikorosho iliyopo yenye uwezo wa kuzalisha katika msimu husika (Crop forecast).
h)Kukusanya taarifa/takwimu za korosho zinazobanguliwa majumbani/vikundi vidogo vya ubanguaji na kuwasilisha Bodi ya Korosho Tanzania.
i)Kuwatambua wadau wa sekta ya kilimo waliopo katika eneo husika la kazi na
kuwaunganisha na wakulima ili kupata huduma wanazotoa.
j)Kuhakikisha kila mkulima ana daftari ambalo litatumika kujaza huduma zitakazotolewa na wadau mbalimbali wakiwemo maafisa ugani kilimo.
k)Kushirikiana na uongozi wa kijiji kuchagua mkulima kiongozi (Lead farmer).
l)Kutoa ushauri kwa mazao mengine yanayolimwa na wakulima wa Kijiji/eneo analosimamia.
m)Kufanya tathmini ya uzalishaji na ubanguaji wa korosho katika eneo lake la kazi kila mwisho wa msimu na kuwasilisha taarifa kwa Bodi ya Korosho Tanzania.
n)Kufanya shughuli nyingine yoyote atakayopangiwa na kiongozi wake.
Sifa zinazohitajika Kijana muhitimu wa fani ya kilimo ngazi ya Stashahada (Diploma) mwenye sifa zifuatazo:-
- Awe mtanzania mwaminifu, mwadilifu, mwenye kujituma na mahusiano mazuri na
wengine. - Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 35.
- Awe amehitimu Stashahada (Diploma) katika fani ya Sayansi ya Kilimo (Agriculture General), Agronomia (Agronomy), Kilimo cha Bustani (Horticulture) au Uzalishaji wa Mazao (Crop Production) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
- Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma.
- Awe hajawahi kufungwa kwa makosa yoyote ya jinai.
- Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa.
- Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba.
- Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika.
- Uzoefu wa kazi katika zao la korosho ni sifa ya ziada.
Namna ya kutuma maombi
Maombi yote yaambatane na
- Vivuli vya vyeti vya kuzaliwa, NIDA, vyeti vya elimu ya sekondari, stashahada na shahada kutoka vyuo vya mafunzo vinavyotambuliwa na serikali (viwe faili moja).
- Picha mbili za hivi karibuni za “passport size” za mwombaji
- Wasifu (Curriculum vitae) wa mwombaji pamoja na anuani kamili, mawasiliano ya simu, barua pepe na anuani za wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
Maombi yote yatumwe kwa Rasi wa ndaki ya Kilimo ya Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo kupitia barua pepe coahr@sua.ac.tz na nakala kwa mkurugenzi- kurugenzi ya Shahada za awali ya chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo .
Waombaji wanashauriwa kutuma maombi yao kupitia barua pepe ingawa wanaweza pia kuleta maombi moja kwa moja kwa ofisi tajwa hapo juu.
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. EA.12/216/01/02
Kwa maelezo zaidi au maswali juu ya tangazo hili tafadhali tupigie kupitia namba zifuatazo: +255760485718
Mwisho wa Kutuma Maombi tarehe 15 Agost 2025.
Tags: NAFASI 50 Za Internship Sokoine University of Agriculture, NAFASI 50 Za Internship Sokoine University of Agriculture 2025/2026
