MAGAZETI ya Leo Jumatatu tarehe 08 September 2025

Filed in Magazetini Leo by on 08.09.2025 0 Comments
Share This Post
MAGAZETI ya Leo Jumatatu tarehe 08 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatatu tarehe 08 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatatu tarehe 08 September 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kamati ndogo (standing committees) mpya zitakazofanya kazi kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili Septemba 7, 2025, na TFF, kamati hizo ni Kamati ya Fedha na Mipango pamoja na Kamati ya Mashindano.

Katika Kamati ya Fedha na Mipango, Athumani Nyamlani ameteuliwa kuwa Mwenyekiti, huku Paul Bilabaye akiwa Makamu Mwenyekiti.

Wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Seif Issa, Dk Seif Muda na Luseshelo Anthony.

Kwa upande wa Kamati ya Mashindano, Hosseah Lugano ataongoza kama Mwenyekiti akisaidiwa na James Mhagama kama Makamu Mwenyekiti.

Wajumbe walioteuliwa ni John Kayombo ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Vedastus Lufano, Isaack Munisi, Kenneth Pesambili, Mhandisi Issa Batenga, Paschal Kihanga na Eliaman Emmanuel.

Rais wa TFF, Wallace Karia amesema kuwa uteuzi huo ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha uwajibikaji na ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za shirikisho hilo.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *