MAJUKUMU ya Msimamizi/Msimamizi Msaidizi wa Kituo Cha Kupigia Kura

MAJUKUMU ya Msimamizi/Msimamizi Msaidizi wa Kituo Cha Kupigia Kura
MAJUKUMU ya Msimamizi/Msimamizi Msaidizi wa Kituo Cha Kupigia Kura
Majukumu ya Msimamizi/Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kupigia Kura ni muhimu kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki, amani na kwa kufuata taratibu.
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa haya hapa ni baadhi ya Majukumu ya Msimamizi/ Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kupigia
✅ Kupokea na Kukagua Vifaa vya Kupigia Kura.
- Kupokea karatasi za kura, orodha ya wapiga kura, mihuri, wino, na vifaa vingine.
- Kuhakikisha vifaa vyote vipo na salama kabla ya kuanza kazi.
✅Kusimamia Ufunguzi wa Kituo.
- Kuweka kituo tayari kwa wakati (saa 1:00 asubuhi).
- Kupanga meza na maafisa wa kituo kwa mpangilio unaofaa.
✅Kuhakikisha Usalama Kituoni.
- Kushirikiana na vyombo vya usalama ikiwa kutatokea vurugu au hali ya sintofahamu.
✅Kuhesabu na Kuandika Matokeo.
- Kufunga kura mwisho wa muda rasmi (saa 10:00 jioni.
- Kusimamia uhesabuji wa kura hadharani.
- Kujaza fomu za matokeo na kuwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.
✅Kutunza Kumbukumbu na Siri.
- Kuhifadhi nyaraka zote kwa usahihi.
- Kudumisha usiri wa taarifa za wapiga kura na matokeo kabla ya kutangazwa rasmi.
✅Kudhibiti Mchakato wa Upigaji Kura.
- Kuthibitisha wapiga kura kwenye daftari la wapiga kura.
- Kusimamia utaratibu wa kupiga kura kwa amani na kwa usiri.
- Kuzuia wizi au udanganyifu wa kura.
✅Kusimamia Maafisa wa Kituo.
- Kutoa maelekezo kwa karani wa kupiga kura, waelekezaji na mlinzi wa kituo.
- Kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa weledi.
Tags: MAJUKUMU ya Msimamizi/Msimamizi Msaidizi wa Kituo Cha Kupigia Kura
