RAIS Samia Suluhu Hassan aapishwa Chamwino Dodoma

Filed in Habari by on 04.11.2025 0 Comments
Share This Post
RAIS Samia Suluhu Hassan aapishwa Chamwino Dodoma

RAIS Samia Suluhu Hassan aapishwa Chamwino Dodoma

RAIS Samia Suluhu Hassan aapishwa Chamwino Dodoma

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Dkt. Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Sherehe zilizofanyika Leo Jumatatu tarehe 3 November 2025.

Mbali ya Rais Samia, Dkt. Emmanuel John Nchimbi naye amekula kiapo cha kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Samia Suluhu Hassan, mwenye umri wa miaka 65, alikula kiapo chake mbele ya Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma, akiahidi “kulinda na kutetea Katiba na umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Sherehe ya kuapishwa kwake imefanyika katika uwanja wa kijeshi katika mji Mkuu wa Dodoma nchini Tanzania.

Dkt. Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju kuwa Rais wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.

Dkt. Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju kuwa Rais wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.

Katika hotuba yake ya kwanza mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa wamesikitishwa na kuhuzunika na matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu.

“Tumesikitishwa na kuhuzunishwa na matukio ya uvunjifu wa amani, upotevu wa maisha na uharibifu wa mali za umma na mali za watu binafsi kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini, hasa kwenye majiji na miji. Kilichotokea hakiendani na taswira na sifa za Kitanzania, na sio Utanzania.” – Rais Samia Suluhu kwenye sherehe ya kuapishwa kuwa Rais, Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan Katika hotuba yake aliziagiza kamati za ulinzi za mikoa, wilaya na kitaifa kuhakikisha shughuli za wananchi za kila siku zinarejea kuanzia Novemba 03, 2025.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *