MFUMO wa Maombi ya Kujiunga VETA (VETMIS)

MFUMO wa Maombi ya Kujiunga VETA (VETMIS)
MFUMO wa Maombi ya Kujiunga VETA (VETMIS)
MWONGOZO WA NAMNA YA KUOMBA MAFUNZO YA MUDA MREFU KWA VYUO VYA VETA 2026 KUPITIA MFUMO WA MAOMBI WA VETMIS
Hatua ya 1: Fungua Kiungo cha Maombi Bonyeza kiungo hiki: https://vetmis.veta.go.tz/fdc
Hatua ya 2: Anza Maombi:
- Ukurasa wa mwanzo (Welcome Page) utafunguka, Bonyeza “Apply” chini ya sehemu ya VETA Long Courses.
Hatua ya 3: Ingia au Jisajili
Mwombaji Mpya: Bonyeza “Register New Account” ili kuunda akaunti mpya.
- Mwombaji Uliyesajiliwa: Weka jina la mtumiaji (Username) na nywila (Password), kisha bonyeza “Login”.
Hatua ya 4: Jisajili Akaunti Mpya
Taarifa Binafsi
Jaza taarifa zifuatazo:
- Jina la Kwanza (lazima)
- Jina la Kati (kama lipo)
- Jina la Mwisho (lazima)
- Namba ya Simu (lazima)
- Barua Pepe
- Mkoa
- Wilaya
- Kata
- Kijiji/Mtaa
Taarifa za Kozi
Chagua: Aina ya Mwombaji:
- Long Course Applicant
- Kituo cha Mafunzo
- Mwaka wa Masomo
Nenosiri
Tengeneza neno la siri kwaajili ya akaunti yako. Ikiwa una maelezo ya ziada, yaweke.
Baada ya kuhifadhi, Username yako itaonekana — ihifadhi vizuri!
Hatua ya 5: Ingia na Kamilisha Maombi
Taarifa Binafsi
- Hakiki taarifa zako
- Weka tarehe ya kuzaliwa na jinsia
- Kitambulisho
Chagua: - Uraia
- Aina ya Kitambulisho
- Namba ya Kitambulisho
- Mahali kilipotolewa
- Tarehe ya mwisho ya matumizi ya kitambulisho
- (Work Permit) kama ipo
Makazi
Thibitisha taarifa zako:
- Nchi
Mkoa - Wilaya
- Kata
- Kijiji/Mtaa
- Mahali pa makazi
- Anwani (kama ipo)
Elimu
Chagua:
- Kiwango chako cha juu cha elimu
- Mwaka uliomaliza elimu hiyo
- Uchaguzi wa Kozi
Chagua kozi kwa kupanga vipaumbele katika sekta na fani (occupation) hadi chaguo tatu.
Taarifa za Ziada
- Chagua ikiwa una uhitaji maalum (kama upo)
- Chagua aina ya mwanafunzi: wa kutwa au bweni
Jaza taarifa za mlezi:
- Majina kamili
- Uhusiano
- Namba ya simu
- Barua pepe (si lazima)
- Anwani
- Maelezo mengine muhimu
Hatua ya 6: Malipo
- Nenda kwenye sehemu ya Bills and Payments
- Bonyeza “Request Control Number” kupata ankara ya malipo (Control
Number) - Lipa kiasi cha TZS 5,000 (kiasi hiki hakitarudishwa) Umefanikiwa!
Subiri matokeo ya uchaguzi kupitia tovuti ya VETA au kupitia vyombo rasmi vya habari.
