FURSA Za Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Muda Mfupi – VETA (YEFFA)

FURSA Za Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Muda Mfupi – VETA (YEFFA)
FURSA Za Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Muda Mfupi – VETA (YEFFA)
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeingia makubaliano ya ushirikiano na taasisi za AMSHA, RUATI, TAMA na MIBOS kupitia Mradi wa Ujasiriamali wa Vijana kwa Mustakabali wa Chakula na Kilimo (Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculture -YEFFA).
Mradi huo unafadhiliwa na AGRA Tanzania na unatekelezwa kupitia vyuo vya VETA vya Kihonda, Manyara, Mpanda na Arusha (Oljoro).
Kupitia mradi huo, vyuo husika vitatoa mafunzo ya muda mfupi katika fani za Agro-mechanics, Umwagiliaji (Irrigation) na Uhifadhi wa Mazao Baada ya Mavuno (Post-harvest).
Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza itaanza tarehe 19/01/2026.
VETA inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi kupitia mradi wa YEFFA.
Mafunzo ni ya kutwa tu (Day Programme).
FANI ZITAKAZOTOLEWA
- Ufundi wa Zana za Kilimo (Agro-Mechanics)
- Umwagiliaji (Irrigation)
- Teknolojia ya Kuhifadhi Mazao Baada ya Mavuno (Post-Harvest Technology).
MIKOA ITAYONUFAIKA NA MAFUNZO
Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Lindi, Morogoro, Pwani, Ruvuma, Njombe, Iringa, Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Katavi, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Songwe na Kagera.
SIFA ZA KUJIUNGA
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Mtanzania mwenye Umri kuanzia miaka 15 na kuendelea.
- Mwenye elimu ya msingi na kuendelea.
UTARATIBU WA KUOMBA
- Maombi yatafanyika kwa njia ya mtandao (online application) kupitia mfumo unaopatikana kupitia tovuti ya VETA: www.veta.go.tz au nakala ngumu za fomu (hardcopy) zinazopatikana kwenye vyuo vya VETA Kihonda, Manyara, Mpanda na Arusha (Oljoro).
- Fomu zote zitatolewa bure kwa kuwa zimegharamiwa na mfadhili.
- Mwombaji anatakiwa kurejesha fomu akiambatisha cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu aliyonayo.
- Fomu zitarejeshwa kwenye chuo husika au kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa maombi.
KIPINDI CHA MAOMBI
Fomu zitatolewa kuanzia tarehe 19 Desemba, 2025 na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 2 Januari, 2026.
ADA NA GHARAMA ZA MAFUNZO
- Gharama za ada tu ya mafunzo zitaalipwa na AGRA kupitia Mradi wa YEFFA.
- Wanawake na watu wenye mahitaji maalum watapewa kipaombele.
Kwa Maelezo na Ufafanuzi zaidi, wasiliana nasi:
VETA Makao Makuu,
12 Barabara ya VETA, 41104 Tambukareli,
S. L. P. 802, Dodoma
Barua pepe: info@veta.go.tz au pr@veta.go.tz Simu ya mkononi: 0755 26 74 89
Tags: FURSA Za Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Muda Mfupi – VETA (YEFFA)
