MFANO wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal

Filed in Makala by on 30.12.2025 0 Comments
Share This Post
MFANO wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal

MFANO wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal

MFANO wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Barua ya kuomba kazi ni waraka ambao mara nyingi husomwa kabla ya waraka mwingine wowote unaoambatanishwa katika uombaji Kazi ambazo ni lazima uandike Barua.

Ni vyema barua hii ikaandaliwa kwa umakini, huku ikijaribu kugusa kwa ufupi mambo yaliyoonekana kwenye wasifu binafsi.

Haya ni Mambo ya Kuzingatia Katika Uandishi wa Barua ya Maombi ya Kazi

Inafahamika kuwa barua rasmi ya kiofisi hufuata kanuni kadhaa kama;

  • Kuwapo kwa anuani mbili. Juu kulia, kuonekana anuani ya mwandikaji isiyotanguliwa na jina na chini kidogo ya anuani hiyo upande wa kushoto mwa barua, huonekana anuani ya mwandikiwa.
  • Huwa na tarehe chini ya anuani ya mwandikaji au juu ya anuani ya mwandikiwa.
  • Tatu, huwa na kichwa cha habari kinachoonyesha lengo, kikitanguliwa na salamu rasmi kama Ndugu, Dear Sir/Madam.
  • Huna sababu ya kutaja jina la mwenye kupokea maombi hayo hata kama unamfahamu kwa jina lake.
  • Barua yako inaelekezwa kwa ofisi, siyo mtu Binafsi.
  • Barua huwa na maelezo yanayofafanua lengo la barua na mwisho huonekana saini na jina la mwandikaji, Fuata kanuni hizo.

Kichwa cha habari kitaje kazi inayoombwa

  • Hakikisha kichwa cha habari kinajitosheleza na kinaeleza wazi wazi kitu gani unachokitaka.
  • Chagua maneno kwa umakini mkubwa kwa sababu wapo wasomaji huishia kusoma kichwa cha habari na kufanya maamuzi.

Mfano,

‘YAH: KUOMBA KAZI YA MHASIBU MSAIDIZI

Hapo msomaji anaelewa kwa uwazi barua inahusu nini. Epuka kutumia maneno yasiyoeleweka au yasiyo rasmi.

Onyesha ulikopata habari za kazi unayoomba

Baada ya kuridhika na kichwa cha habari, ni muhimu sentensi inayoanza chini yake ifanye rejea kwenye tarehe ya tangazo la kazi unayoomba, namba ya kumbukumbu ya tangazo (kama ipo) na mahali tangazo hilo ilipoonekana.

Mfano, “Rejea tangazo la nafasi ya kazi lenye kumbukumbu namba XXX katika gazeti la Mwananchi la tarehe 25 October 2022.”

Wengine wanapenda kuandika sentensi kama, “Kichwa cha habari hapo juu husika”. Haya ni mazoea tu lakini hayana sababu za msingi.

Sema wazi kuwa unaomba kazi

Baada ya kusema ulikopata habari za kazi unayoomba, tumia sentensi inayofuata kueleza nia yako ya kuomba kazi hiyo.

Kumbuka msomaji wa barua hana muda wa kusoma maelezo yako mengi, ni muhimu kuandika kila kitu kwa kifupi na kwa uwazi.

Mfano, “Ninaandika barua hii kuomba kazi ya Uhasibu katika kampuni/shirika au taasisi yako kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo nililolitaja.”

Oanisha majukumu ya kazi na ujuzi ulionao, anza aya mpya kwa kumshawishi msomaji kuwa unaweza kumudu majukumu yaliyotajwa kwenye tangazo lake.

Ili kufanya hivyo, una kazi ya kuoanisha ujuzi, sifa za kitaaluma na uzoefu ulionao na mahitaji ya kazi.

Kabla hujaandika barua, jaribu kuainisha pembeni namna unavyoweza kukidhi sifa zinazotajwa kwenye tangazo na barua yako ionyeshe hivyo.

Vile vile, hakikisha barua yako inajibu kila jukumu lililoonyeshwa kwenye tangazo la kazi.

Hata hivyo, hiyo haimaanishi uandike mambo mengi.

Hitimisha kwa uungwana na ufasaha

Ni vyema kuhitimisha barua yako kwa kuonyesha unavyofaa kwa kazi unayoiomba.

Uchaguzi makini wa maneno kutakupa alama za ziada ikiwa Itaonyesha unavyojua kuwasiliana vizuri.

Kwa mfano, unaweza kusema unatanguliza shukrani zako za dhati na kueleza kwamba uko tayari kuitwa kwenye usaili.

Unaweza kumaliza kwa kutaja nyaraka ulizoambatanisha pamoja na barua hiyo kama vile vivuli vya vyeti, wasifu binafsi na cheti cha kuzaliwa.

Pia, hakikisha lugha unayotumia ni fasaha, inaeleweka na haina makosa ya kiuandishi.

Epuka makosa ya kisarufi kwani yanatoa picha ya mtu mzembe na mvivu, hivyo yanaweza kukugharimu hata kama ni kweli sifa za kitaaluma unazo.

Kumbuka, si sifa za kitaaluma pekee hutumika kufanya maamuzi ya kukuita kwenye usaili.

Aidha, huna haja ya kujitambulisha na kutoa taarifa zisizo za lazima na ambazo ulizitaja kwenye wasifu utakaouambatanisha.

Kwa mfano, haifai kujaza karatasi kwa maelezo kama: “Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 24 nilizaliwa kwenye kijiji cha Mkya wilayani Mjini, Mkoa wa Songea. Nimesoma shule ya Chekechea wilayani Rorya, na kisha nikahamia Kyela kwa masomo ya shule ya msingi mpaka darasa la pili kisha …nikahamia shule ya msingi Samwe, kisha nikaenda….”. Maelezo haya yanaonyesha huna ubunifu wala mbinu za kuwasiliana.

Mwisho na muhimu, ni makosa ya kujitakia kushawishika kutoa taarifa za uongo ili kujenga taswira chanya isiyokuwapo. Uongo una gharama.

Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi

  • Anuani ya mwandishi. Yaani anuani yako wewe unayeandika barua hiyo.
  • Tarehe.
  • Anuani ya anayeandikiwa.
  • Salamu.
  • Kichwa cha habari.
  • Kiini cha barua. Hii ni roho ya barua yako, ukikosea mahali hapa, kama unajibu swali katika mtihani, utapoteza alama, na kama unaomba kazi halisi, utaikosa. Kiini kina aya nne:
  • Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo. Ni katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.
  • Katika aya ya pili, eleza ujuzi wako kwa ufupi. Usieleze sana. Barua hii haipaswi kuwa ndefu kupindukia.
  • Aya ya tatu eleza kwa nini upewe kazi hii wewe na si mtu mwingine. Epuka kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi. Maneno kama, ninaomba kazi hii ili niweze kumtibia mama yangu mgonjwa kitandani, hayana msaada.
  • Aya ya nne eleza uko tayari kwa usahili siku gani?

Mwisho wa barua yako uwe na:

Neno la kufungia. Wako mtiifu. Wako katika ujenzi wa taifa n.k

– Sahihi yako.

– Jina lako

Hii hapa Anwani ya Ajira zote zinazotangazwa Kupitia Ajira Portal

Hii hapa Anwani ya Ajira zote zinazotangazwa Kupitia Ajira Portal

Hii hapa Anwani ya Ajira zote zinazotangazwa Kupitia Ajira Portal.

Zingatia Kuandika Kwa Ufasaha Kwani ukikosea hautaitwa Kwenye Usaili.

Pia hakikisha unasoma barua na CV yako kwa utulivu hadi mwisho kabla hujaituma maombi.

DONWLOAD EXCEL YA BARUA YA KUOMBA KAZI HAPA

DONWLOAD PDF YA BARUA YA KUOMBA KAZI HAPA

Kila la kheri Katika uandaaji wa barua za Kuomba Ajira Serikalini pamoja na Makampuni binafsi.

KUONA AJIRA MPYA BURE KILA SIKU BOFYA HAPA

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *