NAFASI Za Kazi Nsimbo District Council

NAFASI Za Kazi Nsimbo District CouncilNAFASI Za Kazi Nsimbo District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa mamlaka aliyonayo kupitia kifungu cha 31 na 33 cha sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi ya kazi ya kukusanya mapato ya Halmashauri.
✅MKUSANYA MAPATO NAFASI 26
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukusanya fedha kwa niaba ya Halmashauri kwa kuzingatia vyanzo vilivyoainishwa na sheria ndogo za Halmashauri.
- Kuwasilisha fedha yote iliyokusanywa benki kila siku.
- Kuwasilisha ripoti ya makusanyo kwa watendaji wa kijiji au kwa Mkurugenzi Mtendaji au afisa yoyote aliyeidhinishwa.
- Kuwasilisha jina la mtu au kampuni iliyokaidi kulipa ushuru kwa makusudi.
- Kuwaelimisha walipa kodi juu ya umuhimu wa kulipa ushuru kwa hiari bila shuruti.
- Pamoja na klazi nyingine utakazopangiwa na mwajiri wako.
SIFA ZA MUOMBAJI
- Muombaji awe ni Raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
- Awe na uwezo wa kutumia simu janja (smartphone) d) Awe na kitambulisho cha NIDA
MALIPO/POSHO
Malipo/posho ni kiasi cha Shilingi laki mbili (200,000/=) za kitanzania kwa mwezi.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote waambatishe barua za maombi na wasifu binafsi uliojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya Barua pepe (email address) pamoja majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika kama ni waajiriwa wa Serikali waambatanishe nakala za vitambulisho vya Kazi na kama sio mtumishi wa umma awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya isiyopungua milioni 10
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria /wakili ambavyo ni vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
MUHIMU; Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,
S.L.P 688,
MPANDA.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hii HAYATAFANYIWA KAZI.
DONWLOAD PDF HAPA
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16/02/2026
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
