NACTVET Vyuo Vinavyodahili Mkupuo wa Machi 2026/2027

Filed in Elimu by on 13.02.2026 0 Comments
Share This Post
NACTVET Vyuo Vinavyodahili Mkupuo wa Machi 2026/2027

NACTVET Vyuo Vinavyodahili Mkupuo wa Machi 2026/2027

NACTVET Vyuo Vinavyodahili Mkupuo wa Machi 2026/2027

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuufahamisha umma kuwa udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi zote, isipokuwa kozi za Afya Tanzania Bara, umeanza tarehe 10 Februari, 2026 na utakamilika tarehe 28 Februari 2026.

Udahili huu unahusu vyuo vilivyosajiliwa, kuthibitishwa na kuidhinishwa na Baraza kuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi.

Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari pamoja na wahitimu wa vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada wanashauriwa kuwasilisha maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyovipenda.

Waombaji watakaochaguliwa watawasilishwa NACTVET kwa ajili ya uhakiki.

Baraza linaelekeza vyuo kuhakikisha vinazingatia sheria, kanuni na taratibu za udahili, pamoja na kuifuata Kalenda ya Udahili inayopatikana katika tovuti ya Baraza.

Aidha, Baraza linawakumbusha waombaji kuhakikisha wanaomba kujiunga na vyuo vilivyosajiliwa
na kuidhinishwa na Baraza kudahili wanafunzi katika muhula wa Machi, 2026.

Orodha ya vyuo vilivyoruhusiwa kufanya udahili imeambatanishwa hapa chini kwenye PDF.

DONWLOAD PDF YA VYUO HAPA

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *