NAFASI 20 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

Filed in Ajira by on 14.02.2026 0 Comments
Share This Post
NAFASI 20 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

NAFASI 20 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

NAFASI 20 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi za vijana wa kujitolea kama ifuatavyo.

✅DAKTARI II-NAFASI-6

Sifa za Kitaaluma kwa Mwombaji
Shahada ya udaktari kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na serikali waliomaliza internship na kupata usajili kutoka baraza la madaktari Tanganyika (Medical council of Tanganyika).

Majukumu

  • Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na upasuaji wa kawaida na wa dharura.
  • Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
  • Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa
    Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA
  • Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.
  • Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake.
  • Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyopo eneo lake la kazi.
  • Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
  • Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
  • Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality improvement).
  • Kutoa huduma za outreach katika wilaya/Mkoa wake.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu,
    uzoefu na ujuzi wake.

✅AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II (ANAESTHESIA)-NAFASI-3

Sifa za Kitaaluma kwa mwombaji
Stashahada (Diploma) ya uuguzi kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali, waliosajiliwa na baraza la uuguzi na ukunga Tanzania aliyehudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya usingizi na ganzi salama (Anaesthesia)

Majukumu:

  • Kutoa huduma ya usingizi na ganzi salama.
  • Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  • Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II – NAFASI -10

Sifa za Kitaaluma za mwombaji
Stashahada (Diploma) ya uuguzi kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali, waliosajiliwa na baraza la uuguzi na ukunga Tanzania.

Majukumu:

  • Kutoa huduma za uuguzi.
    Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  • Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi.
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅DOBI – NAFASI – 1

Sifa za Kitaaluma kwa mwombaji.
Mhitimu wa kidato cha nne aliyepata mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Service) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

Majukumu

  • Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha.
  • Kutoa taarifa kwa Msimamizi kama nguo imeungua au imepasuka ili ishughulikiwe haraka.
  • Kutunza vifaa vyote vinavyohusika na kazi za udobi.

MALIPO KWA UJUMLA
Malipo ya posho ya posho ya usafiri na chakula yatafanyika kwa kuzingatia mwongozo wa kujitolea katika utumishi wa umma wa mwaka 2025.

MASHARTI YA JUMLA YA MWOMBAJI

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi 35.
  • Awe muhitimu wa elimu ya cheti cha astashahada, stashahada au shahada kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
  • Awe mmiliki halali wa vyeti vya kitaaluma.
  • Awe na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa umma.
  • Awe na barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji wa kijiji/kitongoji/serikali ya mtaa.
  • Awe na utayari wa kujitolea katika eneo husika.
  • Awe hajawahi kuhukumiwa na mahakama kwa makosa ya jinai au nidhamu.
  • Awe na mwenendo na tabia njema inayokubalika na jamii.
  • Awe hajawahi kuajairiwa katika taasisi yoyote ya uma tangu alipohitimu masomo.
  • Kuambatanisha pamoja na maombi nakala za vyeti vilivyohakikiwa na wakili wa serikali, kitambulisho cha taifa/namba ya kitambulisho na/au paspoti ndogo 2 za rangi.
  • Kila mwombaji aandike kwa usahihi Anwani yake na Namba ya simu inayopatikana muda wote kwa ajili ya mawasiliano

Maombi yote yawasilishwe moja kwa moja Ofisi ya Mganga Mfawidhi (Masijala) au yatumwe kwa anwani ifuatayo:-
MGANGA MFAWIDHI,
HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA,
S.L.P 452,
TANGA.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe. 19 Februari, 2026

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *