BEI Mpya Za Mafuta ya Petroli April 2026

Filed in Habari by on 01.04.2026 0 Comments
Share This Post
BEI Mpya Za Mafuta ya Petroli April 2026

BEI Mpya Za Mafuta ya Petroli April 2026

BEI Mpya Za Mafuta ya Petroli April 2026

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 1 APRILI 2026

Mabadiliko ya bei za mafuta nchini kwa mwezi Aprili 2026 yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na vita inayoendelea kati ya Marekani kwa kushirikiana na Israeli dhidi ya Irani iliyoanza tarehe 28 Februari 2026.

Kushambuliwa kwa visima vya mafuta, maghala ya kuhifadhi mafuta na viwanda vya kusafisha mafuta (refineries) pamoja na Irani kufunga Lango la Hormuz linalopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa kwenda kwenye masoko mbalimbali duniani, imeathiri hali ya uzalishaji mafuta kwenye nchi za Mashariki ya Kati ambako Tanzania inaagiza kwa kiasi kikubwa; imeongeza gharama za usafirishaji kutokana na kukosekana kwa meli za kusafirisha mizigo na imeongeza gharama za bima za meli za mizigo kutokana na vita.

Ongezeko hilo la bei za mafuta ni janga la kidunia na Tanzania kama sehemu hiyo inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa upatikanaji wa mafuta nchini na katika bei himilivu ili kupunguza madhara ya kiuchumi na kijamii.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wanashauriwa kutumia mafuta kwa uangalifu na ufanisi mkubwa.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano ya tarehe 1 Aprili 2026 saa 6:01 usiku.

Kwa mwezi Aprili 2026, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia.

BEI Mpya Za Mafuta ya Petroli April 2026

BEI Mpya Za Mafuta ya Petroli April 2026

 

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *