MAGAZETI ya Leo Jumapili 29 June 2025

MAGAZETI ya Leo Jumapili 29 June 2025
MAGAZETI ya Leo Jumapili 29 June 2025


Nyota wa Gambia, Gibril Sillah ametangaza kuondoka Azam FC baada ya kuitumikia kwa miaka miwili.
Mshambuliaji huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuiaga klabu hiyo akisema imekuwa sehemu ya familia yake kwa muda alioichezea.
“Asante Azam FC kwa kila ambacho nyie watu mmenifanyia katika hii miaka miwili. Ni wakati mgumu kwangu kusema kwaheri kwa klabu ambayo nina kumbukumbu nyingi ambazo siwezi kuzisahau katika maisha yangu ya soka.
“Nawashukuru mashabiki wa klabu ambao mara zote wamekuwa na mimi nyakati nzuri na mbaya. Hapana shaka nitaikumbuka klabu hii kwa mengi lakini ndio maisha. Naitakia mafanikio makubwa katik misimu ijayo Inshaa Allah,” ameandika Sillah.
Sillah amesema anatambua mchango mkubwa wa watu ndani ya Azam FC na Watanzania kiujumla.
“Nawashukuru wachezaji, Rais wa klabu, Mtendaji Mkuu, Mwenyekiti, mpishi, Maofisa Habari, Watunza Vifaa, Walinzi, Mama na kila mmoja klabuni kwa kufanya kuishi kwangu kuwe rahisi.
“Na kiukweli nitaikumbuka nchi kubwa ya Tanzania kwa sababu ni taifa la kisoka, kila mmoja anapenda soka kama unacheza Ulaya. Hamasa muda wote iko chanya. Sitosahau kumbukumbu nzudi katika nchi na klabu yangu ya Azam itabakia katika moyo wangu. Naipenda klabu hii. Asante sana Azam FC,” ameandika Sillah.
Katika miaka miwili ambayo Sillah ameitumikia Azam FC, mshambuliaji huyo amecheza idadi ya mechi 68 huku akifunga mabao 21 na kupiga pasi 10 za mwisho katika mashindano tofauti.
