NICKSON Kibabage ni Mnyama

Filed in Michezo, Usajili by on 16.01.2026 0 Comments
Share This Post
NICKSON Kibabage ni Mnyama

NICKSON Kibabage ni Mnyama

NICKSON Kibabage ni Mnyama

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Baada ya mapendekezo ya kocha
mkuu wa Simba Steve Barker aliyehitaji maboresho safu ya ulinzi upande wa kushoto, tayari uongozi umepiga hatua
kuimarisha eneo hilo.

Klabu hiyo imekamilisha usajili wa Mlinzi Nickson Kibabage Kutoka Singida Black Stars FC.

Klabu ya Singida Black Stars Kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii imetoa taarifa ya kukubali maombi kutoka Simba ya kumruhusu mchezaji Nickson Kibabage kujiunga na klabu hiyo.

Baada ya majadiliano, uongozi umeamua kumtoa mchezaji huyo bila malipo.

Singida Black Stars imesema kuwa inaamini katika falsafa ya uendelezaji vipaji hasa kwa wachezaji wazawa.

Uongozi wa klabu hiyo umeona hii ni fursa nzuri kwa mchezaji mzawa kwa kuwa Simba SC inashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Nickson Kibabage ni Mchezaji wa Timu ya Taifa.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *