NAFASI Za Arusha Co-operative Union Limited

NAFASI Za Arusha Co-operative Union Limited
NAFASI Za Arusha Co-operative Union Limited
Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Arusha (ACU Ltd) kinatangaza nafasi mbili (2) za AFISA KILIMO MSAIDIZI.
KAZI ZA AFISA UGANI
- Kuanzisha na kusimamia mashamba ya mfano.
- Kukusanya takwimu mbalimbali za kilimo
- Kusimamia Vyama vya Msingi katika kuandaa mashamba ya Chama.
- Kutoa mafunzo kwa Wakulima kuhusu mbinu bora za kilimo.
- Kutembelea Wakulima shambani.
- Kushirikiana na watafiti wa kilimo na Wadau wengine wa kilimo katika kuongeza uzalishaji wa mazao bora ya kilimo.
- Kusimamia ukusanyaji na tathmini ya takwimu za kilimo.
- Kuandaa mpango wa mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo.
- Kushirikiana na watafiti wa kilimo katika kutoa tahadhari kuhusu viashiria
vya hatari vya magonjwa ya mazao. - Kutoa ushauri wa matumizi ya mbegu bora.
- Kudhibiti visumbufu vya mazao.
- Kuandaa na kuandika mpango kazi wa utekelezaji wa kilimo bora kwa Wakulima kwa kila msimu wa kilimo
SIFA ZA MWOMBAJI.
- Wahitimu wa Kidato cha nne (IV) au Sita (VI) wenye stashahada
(Diploma) ya kilimo au kilimo na mifugo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. - Awe na uzoefu angalau mwaka mmoja kwenye shughuli za kilimo na mifugo.
- Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika taarifa za kazi kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
- Awe na uelewa wa kutumia kompyuta kwa programs za Ms Word, Excel, Power Point, Internet na E-mail.
- Awe na uwezo wa kubuni na kuandika mipango mikakati inayohusu kilimo na ufugaji kwa faida ya wakulima
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo mbalimbali yahusuyo kilimo ama ugani pale anapohitajika.
- Awe na uwezo wa kufasili teknologia ya kisasa ya kilimo na ufugaji kwa wakulima.
- Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana, kufanya kazi na jamii na kuwa na maadili mema.
MASHARTI KWA MUOMBAJI WA NAFASI YA AFISA KILIMO MSAIDIZI
- Muombaji awe ni raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 35.
- Muombaji aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Muombaji aambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini watatu wa kuaminika.
- Maombi yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha Nne na cha sita, kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika, viambatanisho hivyo vibanwe sawasawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Muombaji awe tayari kufanya kazi Mkoa wa Arusha ama Mkoa wa Manyara Wilaya ya Kiteto kwenye shamba la ACU Ltd lililopo Songambele.
- Picha moja ya “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma
Maombi yote yanaweza kuandikwa kwa lugha ya kiingereza au Kiswahili na yatumwe kwa:-
MENEJA MKUU,
CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA MKOA WA ARUSHA, ARUSHA
kupitia barua pepe
recruitment@acu.co.tz
maombi kuwasilishwa kwa njia ya Email ama moja kwa moja katika ofisi za Chama Kikuu cha ACU Ltd zilizopo jengo la ACU mkabala na Maktaba ya Mkoa wa Arusha, Room Na. 103.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 13/08/2025.
Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe hiyo hayatazingatiwa.
Ni Waombaji watakaokidhi vigezo tu ndio watakaotaarifiwa kwa ajiri ya usaili.
