NAFASI Za Kazi Hospitali ya Usangi na Mwanga

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Usangi na Mwanga
NAFASI Za Kazi Hospitali ya Usangi na Mwanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za Ajira ya Mkataba ili waweze kufanya kazi katika Hospitali za Usangi na Hospitali ya Wilaya Mwanga.
✅MTEKNOLOJIA MSAIDIZI RADIOGRAFA – RADIOLOJIA (Radiographer).
SIFA ZINAZOHITAJIKA:
Kuajiriwa wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia Radiografa/Mionzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU:
- Kuwapima wagonjwa wanaolekezwa kwenye eneo lake la kazi.
- Kutunza mitambo na vifaa vya Radiolojia katika eneo lake la kazi.
- Kukagua picha za X-Ray zilizopimwa kwa ubora na kutosheleza (Diagnostic quality).
- Kutunza picha za wagonjwa hadi majibu yanapowafikia Madaktari waliowatuma wagonjwa.
- Kusimamia watumishi walio chini yake.
- Kutoa ushauri kuhusu masuala ya kazi za Radiolojia na Mionzi katika eneo lake la kazi.
- Kuandaa vifaa vya Tiba/Uchunguzi na kusimamia utakasaji vifaa katika eneo lake la kazi (Sterilization).
- Kutoa mafunzo ya awali kwa watumishi wanaopangiwa kazi katika eneo lake la kazi.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
- Kufanya /kusimamia usafi wa chumba cha mionzi.
- Kupokea na kutunza picha za mionzi na madawa ya shughuli za Mionzi.
Ngazi ya Mshahara Ni kwa kuzingatia viwango vya Serikali kwa kima cha chini kwa mwezi. Pamoja na posho nyingine kwa kuzingatia miongozo ya Serikalai.
Kazi ni Mkataba wa Mwaka mmoja (1) na Mkataba utahuishwa kulingana na utendaji kazi mzuri.
MASHARITI YA JUMLA:
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Maombi yote yaambatane
vyeti vya na na taaluma vilivyothibitishwa Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
- Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za Nchi
- Maombi yatakayowasilishwa kinyume au nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Barua za maombi zitumwe Posta S.L.P. 176 MWANGA au ziletwe kwa mkono Ofisi ya Masijala au zitumwe kwa E-mail:ded@mwangadc.go.tz ifikapo au kabla ya tarehe 01/10/2025 saa 9:30 Alasiri.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
