MALIPO na Posho Mpya Za Wanaojitolea 2026

MALIPO na Posho Mpya Za Wanaojitolea 2026
MALIPO na Posho Mpya Za Wanaojitolea 2026
Serikali imeweka utaratibu wa kusimamia malipo na posho kwa Vijana wa Kujitolea wanaofanya kazi ndani ya Taasisi za Umma, kwa lengo la kuhakikisha wanapata msaada wa kujikimu wakati wa kipindi cha kujitolea na kuepusha migogoro ya kiutawala.
- Utumiaji wa vijana wa kujitolea ndani ya Taasisi za Umma utahusisha gharama na rasilimali.
- Hivyo, ni vyema Taasisi za Umma zikahakikisha kuwa zina fedha za kugharamia vijana hawa kabla ya kuingia nao makubaliano ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.
- Ofisi yenye wajibu wa kusimamia Menejimenti ya Utumishi wa Umma itapanga na kuhuisha kiwango cha chini cha malipo ya vijana wa kujitolea ndani ya Utumishi wa Umma.
- Lengo ni kuwezesha Taasisi kupanga bajeti na kuwawezesha vijana wa kujitolea kujigharamia usafiri na chakula.
- Kwa kuanzia, Taasisi zitawalipa vijana wa kujitolea kiasi cha Shilingi 250,000/= kwa mwezi kwaajili ya kugharamia usafiri na chakula.
- Kiasi hiki kitahuishwa kulingana na mazingira, wakati na hali halisi ya uchumi wa Taifa.
- Kwa upande wa posho ya kujikimu, vijana wa kujitolea wanapolazimika kusafiri nje ya vituo vya kazi watalipwa nusu ya posho ya kujikimu inayolipwa mtumishi wa Umma aliyepo katika cheo cha kuingilia katika kada husika.
- Safari za kikazi zifanyike pale inapobidi.
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
