BARAKA Mwangosi Kutua Simba SC

Filed in Michezo by on 15.01.2026 0 Comments
Share This Post
BARAKA Mwangosi Simba SC

BARAKA Mwangosi Simba SC

BARAKA Mwangosi Kutua Simba SC

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Baada ya kuridhishwa na kiwango alichoonyesha kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, klabu ya Simba inatajwa kufungua mazungumzo na Mbeya City kwaajili ya kumsajili mshambuliaji Baraka Mwangosi.

Simba ilimpa Mwangosi nafasi ya
kufanya majaribio visiwani Zanzibar ili kujiridhisha na uwezo wake.

Inaelezwa kuwa benchi la ufundi la Simba linaloongozwa na kocha Steve Barker, limevutiwa na uwezo wake hivyo limeutaka uongozi kuhakikisha unapata saini ya mchezaji huyo wa zamani wa Mbuni FC ya Championship.

Simba inataka kumsajili mshambuliaji huyo kwa lengo la kumtengeneza aweze kuwa sehemu ya kuchukua nafasi ya Suleiman Mwalimu ‘Gomez’ ambaye anacheza kwa mkopo Simba akitokea Wydad ya Morocco.

Mwangosi ni sehemu ya kikosi cha Mbeya City kinachoshiriki Ligi Kuu ya NBC.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *