BEDIA Ikamba Kutua Simba SC

BEDIA Ikamba Simba SC
BEDIA Ikamba Kutua Simba SC
Klabu ya Simba inatajwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji
raia wa DR Congo, Bedia Ikamba,
Kutoka Polisi ya Uganda ambaye ameonyesha ubora katika kufunga mabao pengine zaidi ya Steven Mukwala.
Taarifa zinasema Simba imefanya Mazungumzo na Ikamba ambapo sasa faili la mshambuliaji huyo limepelekwa
kwa kocha Steven Barker akisubiriwa kutoa majibu ya mwisho.
Ikamba mpaka sasa ndiye anayeongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu Uganda, akifunga mabao sita, akilingana na wenzake wawili Patrick Kadu wa Kitara FC na Muhammad Ssenoga (Express) waliofunga idadi kama hiyo.
Hatua ya Simba kuanza kutafuta mshambuliaji mpya imetokana na ripoti ya awali ya kocha Barker ambaye haridhishwi sana na baadhi ya washambuliaji alionao kwenye kikosi hicho.
Taarifa kutoka Simba zinaeleza
Barker anavuta pumzi kwa mshambuliaji mmoja akiwemo Seleman Mwalimu, akitaka kuangalia ubora wake zaidi lakini amepata wasiwasi juu ya ubora wa washambuliaji wengine.
Barker pia anakubali takwimu za Jonathan Sowah lakini akitaka kujaribu kumtengeneza kuona kama anaweza kuwa na utulivu wa kucheza ndani ya eneo la hatari.
