KHADIM Diaw Kutua Simba SC

Khadim Diaw Simba SC
KHADIM Diaw Kutua Simba SC
Klabu ya Simba imetajwa kuwa Katika hatua nzuri Kukamilisha Usajili wa Mlinzi wa kushoto raia wa Mauritania, Khadim Diaw.
Diaw mwenye Umri wa miaka 27 anatua Simba akiwa mchezaji huru baada ya
kuachana na waajiri wake wa zamani Al Hilal FC.
Katika dirisha lililopita, Simba ilifanya jitihada kubwa za kumsajili Diaw lakini Al Hilal hawakuwa tayari kumuachia.
Diaw alikuwa pendekezo la kocha aliyeondoka Fadlu Davids ambapo baada ya kumkosa, akalazimika kumsajili kiraka Naby Camara ambaye anaweza
kutumika kama mlinzi wa kushoto au Kiungo.
