DIARRA Afungiwa na Kutozwa Faini

DIARRA Afungiwa na Kutozwa Faini
DIARRA Afungiwa na Kutozwa Faini
Golikipa wa Klabu ya Yanga, Djigui Diarra amefungiwa kucheza michezo mitatu na kutozwa faini ya Shilingi milioni nne kwa makosa mawili ya kumshambulia Mwamuzi na kuonesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani baada ya mchezo kati Mtibwa Sugar uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Adhabu hiyo imetolewa na Bodi ya Ligi (TPLB) kupitia barua yake rasmi iliyotolewa hii leo Machi 27, 2026 ambapo imeeleza “Katika Mechi Namba 126 ya Mtibwa Sugar FC 1-1 Young Africans SC Mchezaji Djigui Diarra wa Klabu ya Young Africans amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kumshambulia Mwamuzi wa Kati wa mchezo tajwa hapo juu, mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.”
“Mchezaji Djigui Diarra wa Klabu ya Young Africans ametozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuonesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo tajwa hapo juu Diarra ametenda kosa kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.4) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji, kwa sababu kitendo hicho kinaashiria matusi na dharau, adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.”
