NDONGANI Samba Gilbani Kutua Simba SC

Filed in Michezo, Usajili by on 15.01.2026 0 Comments
Share This Post
NDONGANI Samba Gilbani Simba SC

NDONGANI Samba Gilbani Simba SC

NDONGANI Samba Gilbani Kutua Simba SC

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Klabu ya Simba inatajwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati wa Congo Brazzaville, Ndongani Samba Gilbani mwenye Umri wa Miaka 25 Kutoka Asante Kotoko ya Ghana.

Inaelezwa usajli wa beki huyo mahiri ambaye ni nahodha wa Asante Kotoko ni pendekezo la kocha Stave Barker ambaye amehitaji kuongezewa nguvu katika safu yake ya ulinzi.

Wakati Simba ikiendelea kumkosa Abdulrazak Hamza ambaye ni majeruhi huku Rushine De Reuck akirejea baada ya kukosekana kwa wiki kadhaa, Ndongani ambaye pia huitumikia timu ya Taifa ya Congo, anaweza kuwa mchezaji sahihi kuimarisha safu ya ulinzi.

Aidha ujio wake huenda ukamuweka matatani beki raia wa Ivory Coast Caraboua Chamou.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *