JUKUMU la Karani Mwogoza Wapiga Kura

JUKUMU la Karani Mwogoza Wapiga Kura
JUKUMU la Karani Mwogoza Wapiga Kura
Karani Mwongoza Wapiga Kura ana jukumu la kuhakikisha Mpiga Kura anaelekezwa vizuri ndani ya Kituo cha kupigia kura bila usumbufu au mkanganyiko wowote.
Kupitia Makala hii hapa chini tumekuwekea Majukumu Muhimu ya Karani Mwongoza Wapiga Kura
- Kuwapokea wapiga kura wanapofika kituoni.
- Kuwaelekeza wapiga kura kwenye sehemu sahihi kwa utaratibu (mfano: meza ya kuhakiki taarifa, meza ya kupokea karatasi ya kura).
- Kusaidia kuhimili foleni na kuweka mpangilio mzuri wa wapiga kura.
- Kutoa taarifa fupi kwa wapiga kura kuhusu mchakato kwa heshima bila kushawishi.
- Kusaidia watu wenye ulemavu, wazee au wenye mahitaji maalum kufika eneo la kupigia kura.
- Kuhakikisha hakuna mtu anazunguka bila sababu au kuvuruga utaratibu ndani ya kituo.
- Kuwasiliana na msimamizi wa kituo endapo kuna hali ya sintofahamu au tatizo lolote.
Aidha Karani huyu hatoi karatasi ya Kura wala hahesabu kura, yeye ni mratibu wa mtiririko wa wapiga kura, yaani kuhakikisha kila mpiga kura anapiga kura kwa utulivu na kwa utaratibu sahihi.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?AJIRA MPYA KILA SIKU BOFYA HAPA
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
